AS Roma Inamhitaji George wa Chelsea

AS Roma bado wanapigania usajili wa Tyrique George, lakini mpango wa kubadilishana Gimenez-Dovbyk na Milan wapoa tena.

AS Roma Inamhitaji George wa Chelsea

Kuna taarifa zinazoendelea kuripoti kwamba Roma wanatumaini kumsajili Tyrique George kutoka Chelsea siku ya mwisho ya dirisha la usajili, lakini mazungumzo ya mpango wa kubadilishana Santiago Gimenez – Artem Dovbyk na Milan yamepoa tena.

Tayari tumefika kwenye saa 24 za mwisho za dirisha la usajili la majira ya kiangazi, na Giallorossi bado wana mambo mengi ambayo hayajakamilika.

Leo hii unaweza kutusua mkwanja mrefu endapo utacheza michezo ya Kasino ya Mtandaoni kama vile Aviator, Poker, Roullette, Keno, Super Heli na mingine kibao. Ingia Meridianbet sasa na ucheze hapa.

Juhudi za kutafuta winga wa kushambulia zilikwama kwa muda kwa sababu ya Jadon Sancho, lakini baada ya kubainika kwamba hana nia ya kujiunga na Stadio Olimpico, AS Roma wakaachana rasmi na mchezaji huyo wa Manchester United.

AS Roma Inamhitaji George wa Chelsea

Sasa lengo lao ni Tyrique George, na kwa mujibu wa Sky Sport Italia, mazungumzo na Chelsea yamepiga hatua katika saa za hivi karibuni, huku Roma wakitumaini kukamilisha dili hilo kabla ya dirisha kufungwa.

Wakati huo huo, chanzo hicho hicho kimeripoti kwamba mpango wa kubadilishana kati ya Dovbyk na Gimenez umekumbwa na matatizo mapya.

Awali kulikuwa na mwelekeo mzuri baada ya taarifa kadhaa kudai kwamba Gimenez amefungua milango ya kuhamia jana jioni.

Hata hivyo, AS Roma hawajaonyesha hamasa ya kutekeleza mpango huo wa kubadilishana kama Milan, jambo lililothibitishwa na mkurugenzi wa michezo Frederic Massara jana.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.