Ten Hag Afukuzwa na Bayer Leverkusen

Klabu ya Bayer Leverkusen ambayo inakipiga kule ligi kuu ya Ujerumani, BUNDESLIGA imemtimua kazi ambaye alikuwa kocha wao Erik Ten Hag baada ya kukosa matokeo mazuri kwenye mechi mbili alizocheza hadi sasa.

Ten Hag Afukuzwa na Bayer Leverkusen

Kocha huyo kwenye mechi mbili alizocheza, amefanikiwa kupata pointi 1 kati ya 6 huku mechi ya kwanza akipigika akiwa nyumbani na mechi ya pili akitoa sare licha ya mpinzani wake kuwa na kadi nyekundu.

Leverkusen kwenye mechi ya kwanza ambayo walipoteza dhidi ya Hoffenheim wao ndio walitangulia kupata bao kabla ya kufanyiwa comeback na kupoteza wakiwa nyumbani. Lakini mechi ya pili hali ilikuwa hivyo hivyo walianza vyema kwa kuongoza na baadae wakaishia kutoa sare.

Klabu hiyo ilimuajiri Ten Hag akiwa kama kocha huru baada ya kachana na klabu ya Manchester United ambayo waliona kuwa hataweza kuwafikisha kwenye nchi ya ahadi wao kama timu kubwa Uingereza na Duniani kote lakini pia ni klabu yenye mashabiki wengi.

Ten Hag Afukuzwa na Bayer Leverkusen

Bayer Leverkusen msimu uliopita waliishia nafasi ya 2 huku wakifuzu kucheza ligi ya mabingwa msimu huu UEFA hivyo klabu hiyo kutokana na ushiriki wake michuano hiyo imeona kuwa ni vyema kuanza kurekebisha mapema kwani michuano hiyo zinakutana timu zenye ubora kabisa.

Je Leverkusen baada ya kumtimua Ten Hag, msimu huu wanaweza kushika nafasi ya ngapi?. Na je wanaweza kuishia wapi kwenye UEFA ikumbukwe kuwa wachezaji wao ambao walikuwa ni nguzo klabuni hapo akiwemo Wirtz, Frimpong wametimka klabuni hapo.

Leo hii unaweza kutusua mkwanja mrefu endapo utacheza michezo ya Kasino ya Mtandaoni kama vile Aviator, Poker, Roullette, Keno, Super Heli na mingine kibao. Ingia Meridianbet sasa na ucheze hapa.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.