Bayer Leverkusen Washinda Jioooni

Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Ujerumani klabu ya Bayer Leverkusen imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao manne kwa matatu mbele ya klabu ya Wolfsburg katika mchezo mgumu uliopigwa katika dimba la Bay Arena.

Mchezo huu ulianza kwa Bayer Leverkusen kutanguliwa baada ya kuruhusu goli la mapema wakijifunga dakika ya tano ya mchezo kupitia beki wao Mukiele, Lakini mabingwa hao watetezi wa ligi kuu Ujerumani walisawazisha dakika ya 14 kupitia kwa kiungo wao Florian Wirtz kabla ya Jonathan Tah kuwapa uongozi dakika ya 32 ya mchezo.bayer leverkusenKabla ya kipindi cha kwanza kumalizika Wolfsburg walieka mzani sawa kwa kusawazisha bao kupitia kwa Bornauw dakika ya 34, Kabla ya dakika ya 45 wageni kupata bao la tatu kupitia kwa kiungo Mattias Svanberg na mchezo huo kwenda mapumziko kwa Leverkusen kua nyuma ambapo Wolfsburg wakiongoza 3-2.

Kipindi cha pili vijana wa Xabi Alonso walikuja na kwa mkakati wa kuhakikisha wanasawazisha goli na hata kufanikiwa kupata matokeo ya ushindi, Ambapo dakika ya 48 tu ya mchezo mchezaji Hincapie aliipatia Leverkusen bao la kusawazisha na kazi ikawa kupata goli la ushindi ili waweze kushinda mchezo huo.bayer leverkusenKama ilivyo kawaida yao dakika za jioni kabisa Victor Boniface alifanikiwa kuiandikia Bayer Leverkusen bao ushindi mnamo dakika ya 93 ya mchezo na kuihakikishia klabu hiyo alama tatu, Klabu hiyo imekwea mpaka nafasi ya pili ya msimamo wa ligi hiyo wakiwa na alama 9 kwenye michezo minne waliyocheza mpaka sasa.

Acha ujumbe