Simba Yatinga Hatua ya Makundi Shirikisho Kibabe

Klabu ya Simba imefanikiwa kufuzu harua ya makundi ya kombe la shirikisho barani Afrika kibabe kabisa baada ya kuifunga klabu ya Al Ahly Tripoli kwa jumla ya mabao matatu kwa moja katika uwanja wa Benjamin Mkapa.

Klabu ya Al Ahly Tripoli ambao walikua wageni walianza kupata goli la mapema kupitia kwa mshambuliaji wao raia wa kimataifa wa Angola Mabululu dakika ya 17 tu ya mchezo, Lakini wekundu wa msimbazi walirejea mchezoni na kuweza kusawazisha bao hilo kupitia kwa mchezaji Kibu Dennis dakika ya 36 kabla ya Leonel Ateba kuweka bao la pili dakika ya 45 ya mchezo.simbaWekundu wa Msimbazi walikwenda mapumziko wakiwa wanaongoza kwa mabao mawili kwa moja jambo ambalo liliwashusha presha klabu hiyo, Kwani kabla ya kusawazisha bao walionekana kua na presha kubwa kwani walikua wakihitaji ushindi kwa kiwango kikubwa katika mchezo huu.

Kipindi cha pili klabu ya Simba ilionekana kuendelea na moto ambao walikua nao mwishoni mwa kipindi cha kwanza ambapo walipata bao la tatu dakika ya 62 ya mchezo kupitia kwa Leonel Ateba japo lilikataliwa, Lakini dakika za jioni kabisa Edwin Balua aliwapatia wekundu wa msimbazi bao la tatu.simbaKlabu ya Simba wanaendelea kudhihirisha ubora wao kwenye michuano mikubwa barani Afrika kwani ndani ya miaka sita wamefanikiwa kwenda hatua ya makundi barani Afrika mara tano, Shirikisho mara mbili huku ligi ya mabingwa mara tatu hii inakupa picha kua klabu hiyo imeweka viwango kwenye soka la Afrika.

Acha ujumbe