Bayern Leverkusen Kulinda Rekodi Mbele ya Atalanta Leo??

Klabu ya Bayern Leverkusen leo itashuka dimbani kumenyana na klabu ya Atalanta ya nchini Italia katika mchezo fainali ya Uefa Europe League utakaopigwa kule nchini Ireland katika jiji la Dublin.

Bayern Leverkusen mabingwa wapya wa ligi kuu ya Ujerumani wamekua na msimu mzuri sana katika michuano yote ambayo wamekua wakishiriki kwani hawajafanikiwa kupoteza mchezo hata mmoja mpaka sasa.BAYERN LEVERKUSENSwali gumu ambalo wengi wanajiuliza leo je vijana wa kocha Xabi Alonso wataweza kulinda rekodi yao ya kutokufungwa mchezo wowote msimu huu mbele ya vijana wa kocha Gian Pierro Gasperrini. Hapo ndipo utamu wa fainali ya michuano hiyo unaposubiriwa.

Mchezo unatarajiwa kua na mvuto mkubwa sana kwani licha ya kua fainali lakini pia mchezo unakwenda kukutanisha timu mbili ambazo zinafundishwa na makocha wanaoaminika kua bora sana kwenye mbinu. Atalanta akiwa kocha Giann Pierro Gasperrini huku Bayern Leverkusen akisimama Xabi Alonso hivo utakua mpambano mkali wa kimbinu.BAYERN LEVERKUSENKubwa zaidi ambalo linasbiriwa kwa hamu kubwa ni kama Atalanta watakwenda kuzuia rekodi ya klabu ya Bayern Leverkusen kucheza michezo 51 bila kupoteza mpaka sasa kwenye michuano yote msimu huu, Au vijana wa Xabi Alonso wataendeleza rekodi yao na kuitafuta rekodi ya kutofungwa kwenye michuano yote msimu ikiwa na maana watatwaa mataji matatu bila kupoteza mchezo.

 

 

Acha ujumbe