Rodri Apata Majeraha Dhidi ya Arsenal

Kiungo wa klabu ya Manchester City Rodri amepata majeraha ya goti katika mchezo dhidi ya Arsenal ambao unapigwa katika dimba la Etihad kitendo ambacho kimemfanya kutolewa nje ya uwanja na kushindwa kuendelea na mchezo.

Kiungo Rodri ambaye alikosekana katika kikosi cha City kwa wiki kadhaa za mwanzo wa msimu kutokana na kusumbuliwa na majeraha kama ilivyoripotiwa, Baada ya kurejea kwenye mchezo wa Inter Milan leo ulikua ni mchezo wake wa pili tangu arejee uwanjani na bahati mbaya imekua upande wake baada ya kupata tena majeraha.rodriHaijafahamika bado kiungo huyo wa kimataifa wa Hispania atakaa nje ya uwanja kwa muda gani ripoti ya madaktari ndnai ya klabu ya Manchester City inasubiriwa kutoa taarifa hiyo, Lakini kama inavyofahamika jeraha la goti mara nyingi huwaweka wachezaji nje kwa kipindi kirefu.

Klabu ya Manchester City itakua imepata pengo kubwa kama kiungo Rodri atakua nje ya uwanja kwa muda mrefu kwani mchezaji huyo amekua mhimili kwenye kikosi cha kocha Pe Guardiola kwa misimu takribani mitatu sasa, Hivo kukosekana kwake lazima litakua pengo kubwa kwa mabingwa hao watetezi wa ligi kuu ya Uingereza.

Acha ujumbe