Thuram Adai Inter Walikosa Bahati Kwenye Kichapo Kigumu Dhidi ya Udinese

Inter imepoteza mechi yake ya kwanza ya msimu huu usiku wa jana baada ya kukubali kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Udinese waliocheza kwa ari kubwa na kugeuza matokeo kutoka nyuma, na kuishtua timu ya Cristian Chivu huku Thuram akisema kuwa hawakustahili.

Thuram Adai Inter Walikosa Bahati Kwenye Kichapo Kigumu Dhidi ya Udinese

Akizungumza na Inter TV baada ya mchezo (kupitia FCInterNews), mshambuliaji wa Nerazzurri, Marcus Thuram, alionekana mtulivu akisema, “Hatuwezi kukata tamaa, tulizungumza vizuri ndani ya chumba cha kubadilishia nguo.”

Thuram alikubali kuwa wao kama timu walijua mechi hiyo ingekuwa ngumu, baada ya kuona Udinese wakionyesha ubora dhidi ya finalisti wa Ligi ya Mabingwa msimu uliopita, “Tulijua ingekuwa mechi ngumu. Katika msimu kuna michezo migumu kama hii.”

Leo hii unaweza kutusua mkwanja mrefu endapo utacheza michezo ya Kasino ya Mtandaoni kama vile Aviator, Poker, Roullette, Keno, Super Heli na mingine kibao. Ingia Meridianbet sasa na ucheze hapa.

Mfaransa huyo alitoa pasi ya bao kwa Denzel Dumfries aliyefunga bao la kwanza, kabla ya Udinese kufunga magoli mawili ya kushtukiza na kuiacha San Siro ikiwa kimya kwa mara ya pili ndani ya wiki moja baada ya wapinzani wao wakubwa, AC Milan, kufungwa mechi ya ufunguzi na Cremonese ya Davide Nicola.

Thuram Adai Inter Walikosa Bahati Kwenye Kichapo Kigumu Dhidi ya Udinese

Licha ya kichapo hicho, Thuram alibaki na mtazamo chanya akisema, kipindi cha pili walifanya mashambulizi sana lakini hawakuwa na bahati. Aliongez akusema kuwa lazima waanze mechi kwa namna walivyoanza kipindi cha pili kwa kucheza hivyo wanaweza kubadili hali ngumu kuwa ushindi.

“Kipindi cha pili tulisukuma sana lakini hatukuwa na bahati. Ni lazima tuanze mechi kwa namna tulivyoanza kipindi cha pili, kwa kucheza hivyo tunaweza kubadili hali ngumu kuwa ushindi.”

Sasa Nerazzurri watalazimika kutumia mapumziko ya michezo ya kimataifa kurekebisha makosa yao na kujiandaa kwa ratiba ngumu ya mwezi Septemba, wakikabiliwa na michezo sita ndani ya wiki mbili pekee, ikiwemo safari za kukutana na Juventus na Ajax.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.