Lamptey Ajiunga na Fiorentina Akitokea Brighton

Klabu ya Fiorentina imethibitisha kumsajili beki wa pembeni Tariq Lamptey kwa uhamisho wa kudumu akitokea Brighton & Hove Albion.

Lamptey Ajiunga na Fiorentina Akitokea Brighton

Kwa mujibu wa taarifa, mtaalamu wa usajili wa Football Italia, Alfredo Pedullà, aliripoti kwa kipekee kwamba Fiorentina na Brighton walifikia makubaliano siku ya Jumamosi.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ghana amekamilisha uhamisho wa thamani ya €6 milioni pamoja na nyongeza kadhaa (add-ons).

Lamptey alizaliwa Hillingdon, England, Septemba 30, mwaka 2000. Alipitia kwenye mfumo wa vijana wa Chelsea kabla ya kuhamia Brighton, ambapo katika misimu mitano iliyopita amecheza mechi 122 kwenye Premier League, Europa League, FA Cup na EFL Cup, akifunga magoli matano na kutoa pasi 12 za mabao.

Lamptey Ajiunga na Fiorentina Akitokea Brighton

Fiorentina imeanza msimu mpya wa Serie A kwa sare mbili mfululizo ugenini dhidi ya Cagliari na Torino, lakini tayari imefuzu hatua ya makundi ya UEFA Conference League, michuano ambayo itashiriki kwa msimu wa nne mfululizo.

Lamptey ni beki wa pembeni mwenye uwezo wa kucheza kulia au kushoto, jambo linalomaanisha atakuwa na ushindani wa namba na Robin Gosens pamoja na Dodo katika dimba la Stadio Artemio Franchi.

Kwa mujibu wa vyanzo vya Football Italia, Lamptey mwenye umri wa miaka 24 amesaini mkataba wa miaka minne na Fiorentina.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.