As Roma nao Waivunja Girona

Klabu ya As Roma nao wamekua moja ya vilabu kadhaa barani ambavyo vimehakikisha vinaivunja klabu ya Girona ya nchini Hispania ambayo ilifanikiwa kufanya vizuri sana msimu uliomalizika.

As Roma wako kwenye hatua za mwisho kabisa kukamilisha usajili wa mshambuliaji Artem Dovbyk ambaye alikua anaitumikia klabu ya Girona msimu uliomalizika na kufanikiwa kufanya vizuri sana ndani ya klabu hiyo, Huku akimaliza kama mfungaji bora wa ligi kuu ya Hispania.as romaMiamba ya soka kutoka nchini Italia walikua wanatafuta mshambuliaji sokoni ambaye ana ubora mkubwa kwakua mshambuliaji ambaye alikua klabuni kwao ni Romelu Lukaku ambaye ni mchezaji wa Chelsea na alikua kwao kwa mkopo, Hivo hiyo imewafanya kuamua kwenda kwa Artem Dovbyk ambaye amekua na msimu bora sana ndani ya timu yake.

Artem Dovbyk mfungaji bora wa ligi kuu ya Hispania msimu wa 2023/24 jambo ambalo lilifanya vilabu kadhaa kuanza kuwinda saini yake kwenye dirisha hili kubwa, Lakini ni As Roma ambao wanaonekana kuokota dodo kwakua mpaka sasa klabu hiyo ipo kwenye hatua za mwisho kukamilisha usajili wa mshambuliaji huyo.

Acha ujumbe