Crystal Palace Inaendelea Kujiimarisha

Klabu ya Crystal Palace inaendelea kuhakikisha inaboresha kikosi chao kuelekea msimu ujao ambapo klabu hiyo ipo mbioni kukamilisha usajili wa winga wa kimataifa wa Senegal Ismael Sarr.

Crystal Palace ilikua inafukuzia huduma ya kiungo wa klabu ya Arsenal Eddie Smith Rowe lakini wakazidiwa na klabu ya Fulham ambao ndio wameshinda vita hiyo, Lakini wao mpaka sasa wana uhakika wa kupata huduma ya winga Ismael Sarr ambaye alikua anakipiga klabu ya Olympique Marseille ya Ufaransa.crystal palaceWinga Ismael Sarr mpaka sasa inataarifiwa amemaliza vipimo vya afya ndani ya klabu hiyo na ni wazi klabu hiyo kutoka jiji la London wameshakamilisha usajili wa winga huyo kuelekea msimu ujao ambapo wanataka kuhakikisha wanaendelea pale walipoishia msimu uliomalizika.

Klabu ya Crystal Palace imekua na msimu bora sana wa mwaka 2023/24 chini ya kocha Glasner ambaye aliikuta klabu hiyo kwenye hali mbaya, Lakini alifanikiwa kuirejesha kwenye ubora ndani ya wakati mfupi  na kuifanya klabu hiyo kua moja ya timu za daraja la kati zilizofanya vizuri msimu uliomalizika na usajili wao unaonesha wanataka kuendelea kubaki kwenye kiwango bora.

Acha ujumbe