Joshua Mutale na Mukwala Watoa Neno Simba

WACHEZAJI wa Simba Joshua Mutale winga na Steve Mukwala Mshambuliaji wamefunguka kuelezea namna ambavyo kambi ya timu hiyo ilivyokuwa huko Ismailia Misri. Jisajili hapa kuwa wa kwanza kushinda Mamilioni ya Meridianbet kila siku.

Akizungumzia kikosi chao, Joshua Mutale alisema walikuwa na muda mzuri Misri kujiweka sawa tayari kwa msimu mpya huku akidai kuwa wamejengeka kimwili na kiushindani.

Alisema wamepata utimamu wa mwili vizuri na wapo tayari kwa kushindana huku akifurahia namna wachezaji wenzake walivyo na muunganiko mzuri.

Beti na Meridianbet kwa ushindi mkubwa na odds kubwa, Ligi  zinakaribia kuanza,  usije kupishana na gari la Mshahara.

Kwa upande wa Steve Mukwala ambaye alifunga goli moja kwenye mchezo wa mwisho wa kirafiki alisema, walikuwa na maandalizi mazuri na ameona namna wachezaji wenzake walivyokuwa wanapambana kusaka nafasi kikosi cha kwanza.

“Kwa upande wetu kama wachezaji tunafikiri kuna kitu tumeongeza hasa kwenye mechi tatu tulizocheza, mashabiki wajitokeze kwa wingi kuona timu yao Jumamosi katika Simba Day, nawaahidi kuwa watafurahi,” alisema.

Katika mechi tatu walizocheza Simba wakiwa Misri, wamefunga mabao saba na kuruhusu mawili. Wafungaji wao ni Mutale, Mukwala, Mashaka, Ladack Chasambi, Augustine Okejepha na Charles Ahoua aliyepiga mbili.

Michezo ya Kasino na Sloti ni machimbo yanayotoa pesa kirahisi. Cheza kasino hapa.

Acha ujumbe