Klabu ya As Roma inaelezwa imejipanga kujiandaa kufanya mazungumzo na klabu ya Chelsea kwajili ya mshambuliaji wa klabu hiyo raia wa kimataifa wa Ubelgiji Romelu Lukaku.
Wamiliki wa klabu ya Chelsea wanaelezwa wapo tayari kwajili ya mazungumzo na klabu ya As Roma kwajili ya mchezaji Romelu Lukaku, Lakini kuna baadhi ya vipengele wanataka vitimizwe ili waweze kumuachia mchezaji huyo kwa mkopo.
Chelsea wapo tayari kumuachia Lukaku kwa mkopo lakini watahitaji kiwango fulani cha pesa kutoka kwa klabu ambayo itamuhitaji mchezaji huyo lakini pia klabu hiyo ihakikishe inamlipa mshahara mchezaji huyo ili wamuachie.
Mshambuliaji Romelu Lukaku alikua anakaribia kutua ndani ya klabu ya Juventus ambao walikua wameonesha nia ya kutaka kumsajili mchezaji huyo,Lakini mashabiki wa klabu hiyo walionesha kutomuhutaji mchezaji huyo ndipo mpango huo ukafa.
Mabosi wa As Roma kama watafanikiwa kutimiza matakwa ya kimkataba ya klabu ya Chelsea juu ya mchezaji Romelu Lukaku basi wanaweza kumpata mchezaji huyo kwa mkopo na kuweza kuboresha kikosi chao.


