Kevin de Bruyne Ampa Maua yake Bruno

Kiungo wa klabu ya Manchester City Kevin de Bruyne amempa maua yake kiungo wa klabu Manchester Bruno Fernandes kwa kusema kiungo huyo ni kiungo mashine kwenye utengenezaji wa nafasi.

Kevin de Bruyne wakati anafanya mahojiano na mwanahabari aliwekewa viungo watatu ambao ni Bruno Fernandes wa Man United Martin Odegard wa klabu ya Arsenal na James Maddison anayekupiga Tottenham kwasasa na kusema Bruno ni hatari kwenye kutengeneza nafasi.KEVIN DE BRUYNEKiungo wa klabu ya Manchester United Bruno Fernandes amekua moja ya viungo wanaofanya vizuri ndani ya ligi kuu ya Uingereza tangu afike hapo, Ndipo kiungo huyo wa kimataifa wa Ubelgiji alipoamua kumpa maua yake kiungo huyo.

Kiungo wa klabu ya Manchester City baada ya kusema Bruno ni mashine kwenye suala la utengenezaji wa nafasi lakini pia alisema kiungo Martin Odegard ni kiungo mzuri ila ni bora sana kwenye kuumiliki mchezo, Huku akisema Maddison anahitaji muda zai kuonesha zaidi akiwa kwenye klabu kubwa.KEVIN DE BRUYNEKiungo Bruno Fernandes alikua kiungo alietengeneza nafasi nyingi zaidi katika ligi kuu ya Uingereza na hii inamaanisha kiungo wa klabu ya Manchester City Kevin de Bruyne alikua sahihi kusema kiungo huyo wa kimataifa wa ureno ni mashine kwenye kutengeneza nafasi.

Acha ujumbe