Kevin de Bruyne Kukosekana Miezi Kadhaa

Kiungo wa klabu ya Manchester City Kevin de Bruyne inaarifiwa atakosekana kwa miezi kadhaa akiwa nje ya uwanja baada ya kupata majeraha katika mchezo dhidi ya Burnley.

Kevin de Bruyne alipata majeraha katika mchezo dhidi ya Burnley ambao ulipigwa siku ya ijumaa ambapo majeraha yake hayakuchukuliwa kama makubwa sana, Lakini taarifa zinasema kua atakua nje ya uwanja kwa miezi kadhaa.kevin de bruyneKocha Pep Guardiola wakati akizungumzia suala kiungo huyo amekiri pia watamkosa kiungo huyo kwa muda kidogo,Kwani kiungo anaweza kufanyiwa upasuaji siku kadhaa zijazo na hii ndio itasababisha kumuweka nje kwa muda mrefu.

Mchezaji huyo amekua moja ya wachezaji muhimu sana kwenye kikosi cha Manchester City tangu amejiunga na klabu hiyo, Lakini kuanzia msimu uliomalizika amekua akiandamwa na majeraha ya mara kwa mara.kevin de bruyneKiungo Kevin de Bruyne mbali na kua mchezaji muhimu kwenye kikosi cha Manchester City, Lakini pia alikua moja ya wachezaji waliotumika zaidi kwenye kikosi hicho hivo ni wazi inaweza kua sababu inayopelekea kupata kwake majeraha kwasasa mara kwa mara.

Acha ujumbe