Lavia Njiani Kuelekea Chelsea

Aliyekua kiungo wa klabu ya Southampton Romeo Lavia yuko mbioni kujiunga na matajiri wa jiji la London klabu ya soka ya Chelsea kwa ada ya uhamisho wa paundi milioni 50.

Kiungo Romeo Lavia alishaweka wazi tangu jana kua anataka kwenda klabu ya Chelsea, Kwani ndani ya klabu hiyo ndio anaona mustakabali wa maendeleo yake ya soka kwa siku zijazo kulinganisha na vilabu vingine vilivyokua vikimtaka.LaviaKlabu ya Chelsea inaendelea kuboresha eneo lake la katikati kwani jana walifanikiwa kumtambulisha kiungo Moises Caicedo na leo wako mbioni kumalizana na kiungo mwingine kijana raia wa kimataifa wa Ubelgiji.

Kiungo huyo wa kimataifa wa Ubelgiji ambaye amekulia akademi ya Manchester City alikua moja ya wachezaji muhimu kwenye kikosi cha Southampton msimu uliomalizka licha ya klabu hiyo kushuka daraja.LaviaChelsea wao wameendelea kuonesha umwamba mbele ya klabu ya Liverpool baada ya kuwapokonya wachezaji wao wawili ambao walikua wanawawania kwani Caicedo alikua anahitajika na Liverpool vilevile Romeo Lavia lakini wote wameenda klabu ya Chelsea.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.