Ligi ya Tanzania Bara kuendelea hii leo ambapo matajiri wa jiji la Dar es salaam Azam fc watakuwa ni wageni wa Mbeya City ya mkoani Mbeya ambapo watakuwa wakicheza michezo yao ya raundi ya nne.

 

Azam Kuzichapa na Mbeya City

Wanalamba lamba hao ambao  wanashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika msimu huu wenyewe  hawajaanzia hatua ya mwanzo kama Geita Gold watakuwa ni wageni katika Sokoine Stadium kuvaana na Mbeya City.

Azam ambae siku si nyingi imemtangaza kocha mpya baada ya kumtimua aliyekuwa kocha wake Abdihamid Moalin na sasa kuna kocha wa Kifaransa ambaye ameichukua timu hiyo huku hii ikiwa ni mechi yake ya kwanza akiwa na timu hiyo ambapo mechi iliyopita ambayo walicheza dhidi ya Yanga na kutoa sare ya 2-2  alikuwa kama mtazamaji, ndani ya mechi tatu Azam walizocheza wameshinda moja na sare mbili.

 

Azam Kuzichapa na Mbeya City

Wakati kwa upande wa Mbeya City wao ndani ya mechi hizo tatu walizocheza wameshinda mechi moja, wametoa sare mechi moja na wamepoteza mchezo mmoja huku tofauti yao ikiwa ni alama moja tu, Hivyo mechi hii kila mtu anahitaji alama 3 ili aweze kujihakikishia usalama kwenye msimamo maana wanasema biashara asubuhi jioni mahesabu.

 

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa