Rais wa Barcelona Joan Laporta inasemekana kuwa anatamani sana aliyekuwa mchezaji wao wa muda mrefu klabuni hapo Lionel Messi amalize soka lake katika klabu yake ya muda mrefu.

 

Barcelona Wanapanga Kumrudisha Messi Barcelona.

Mshezaji huyo wa Kimataifa wa Argentina mwenye miaka 35, aliondoka Camp Nou mnamo Agosti mwaka jana kutokana na matatizo ya kifedha yaliyokuwa yanaikumba timu hiyo na kushindwa kumbakiza klabuni hapo.

Messi alijiunga na Barcelona mwaka 2000 na alishirikiana na klabu hiyo kwa zaidi ya miongo miwili, akifunga mabao 672 katika mechi 778 alizoanza katika klabu hiyo huku Rais wa klabu hiyo akipanga kumrejesha tena Nou Camp.

Kwa mujibu wa Sport, inasemekana kuwa klabu inataka kufanya uhamisho huo dirisha dogo la usajili la kumnunua gwiji wa klabu hiyo, kwa kuchukua fursa ya hali ya Fair Play mwezi huo, badala ya kusubiri msimu dirisha kubwa.

Barcelona Wanapanga Kumrudisha Messi Barcelona.

Hata hivyo, mpango wa Laporta umejaa vikwazo kwa Barcelona kushinda, bila kusahau vikwazo vya kifedha vya LaLiga, pamoja na kumshawishi Messi na klabu yake ya sasa ya Paris Saint-Germain kuachana katikati mwa msimu.

Messi amesema hadharani kuwa ameahirisha maamuzi yoyote kuhusu klabu yake au mustakabali wa Kimataifa hadi baada ya Kombe la Dunia. Lionel katika timu yake ya sasa amekuwa na mchango mkubwa sana ambapo mpaka sasa amecheza mechi 38, amefunga mabao 13 na ametoa pasi za mabao 24.

Barcelona Wanapanga Kumrudisha Messi Barcelona.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa