LEO Jumapili, bendera ya Tanzania itapepea tena kwenye ulimwengu wa soka la wanawake Afrika, wakati ambapo Simba Queens watashuka dimbani kucheza mchezo wa ufunguzi na mwenyeji wa mashindano hayo AS FAR Rabat ya Morocco, mchezo utakaopigwa majira ya Saa 10:00 Usiku.

Huo, utakuwa ni mchezo wa kufungua dimba kwa timu hiyo kwenye kundi A la Ligi ya Mabingwa Afrika na watacheza na timu mwenyeji wa nchi hiyo ambao pia ni mshindi wa tatu wa Ligi ya Mabingwa Afrika msimu uliopita.

 

Simba Kukipiga Leo Morocco

Nahodha wa Mabingwa hao Opah Clement wakati timu hiyo ikielekea Morocco alizungumza kuwa wanataka kulipa kile ambacho Serengeti Girls wamekifanya kombe la dunia kwa kufika robo fainali, akisema Simba itafika hadi nusu fainali au zaidi.

Kocha wa timu hiyo Charles Ayiekho, alisema kuwa ameshazifuatilia timu zote na kujua nani ni mchezaji hatari kwa upande wa wapinzani wao na kuongeza kuwa analijua soka la Afrika na yupo kwenye kazi ya ukocha kwa zaidi ya miaka 20.

 

Simba Kukipiga Leo Morocco
Nahodha wa Simba Queens-Opa Clement

Matumaini ya watanzania wengi ni kuiona timu hiyo inafanya vizuri kwenye mashindano hayo ya Ligi ya mabingwa barani Afrika kwa timu za wanawake, ikiwa Simba amepangwa kundi A, dhidi ya wenyeji AS FAR.

Baada ya mchezo huo Mabingwa hao watapata siku mbili za kufanya mazoezi kabla ya kushuka dimbani kuikabili Determine Girls ya Libya, November 02, 2022. Itacheza tena mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi November 05, 2022 kwa kuikabili Green Buffalos ya Zambia.

Michuano hiyo inajumuisha timu nane zilizopangwa katika Makundi mawili ambapo kila kundi litatoa timu mbili zitakazofuzu hatua ya Nusu Fainali ya Michuano hiyo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa