Chelsea wameripotiwa kumfanya beki wa kati wa Monaco, Benoit Badiashile kuwa mlinzi wao mkuu katika dirisha la usajili la Januari.

Wamekuwa wakihusishwa sana na RB Leipzig na kinara wa Croatia Josko Gvardiol, lakini Fabrizio Romano anaamini kuwa Chelsea italazimika kuvunja rekodi ya ada ghali zaidi ya uhamisho iliyolipwa kwa beki ili kufanikisha dili.
Badala yake, klabu hiyo ya Stamford Bridge inasemekana kumpigia debe Badiashile mwenye umri wa miaka 21 wa Monaco, ambaye amecheza mechi 106 tangu aanze kucheza mechi yake ya kwanza akiwa na umri wa miaka 17
Badiashile pia alipata mechi zake za kwanza za wakubwa kwa Ufaransa mwaka huu, akicheza dakika 90 kamili katika mechi za UEFA Nations League mwezi Septemba dhidi ya Austria na Denmark kabla ya kukosa kikosi cha Kombe la Dunia.

Huku ikiwa imesalia zaidi ya miezi 18 katika mkataba wake, Monaco watahitaji kuamua ikiwa wanaweza kumfunga kwa mkataba wa muda mrefu, la sivyo unaweza kuwa wakati wa kumlipa.
Kwa mujibu wa The Athletic, Badiashile ni mchezaji ambaye amekuwa kwenye rada za Ligi Kuu kwa muda mrefu, akibainisha dau la pauni milioni 22 kutoka Manchester United mwaka 2020.
Ripoti hiyo inadai kwamba Badiashile hakuwa na haraka ya kuondoka wakati huo kwani tayari alikuwa kwenye kikosi cha kwanza, lakini amefunguka na kuwa na wazo la kusonga mbele ili kuchukua hatua nyingine ya maisha yake ya soka.

Chelsea wanasemekana kuandaa ofa ya pauni milioni 35 kwa ajili ya mchezaji huyo ambaye ana uzoefu wa kucheza nafasi ya beki ambayo inaweza kuwa chini ya nusu ya bei inayotarajiwa kwa Gvardiol.

