Ligi kuu ya Uingereza EPL inarejea hii leo ambapo vijana waJurgen Kloop Liverpool watakuwa ugenini kumenyana dhidi ya Aston Villa majira ya saa 2:30 usiku.

Liverpool ambao msimu uliopita walimaliza nafasi ya pili, lakini mpaka sasa nafasi ya kutetea taji hilo inaonekana hafifu kutokana na mwendelezo wa matokeo ambayo wamekuwa wakiyapata katika mechi zao.
Kabla ya mapumziko ya Kombe la Dunia Majogoo walipata ushindi wao mnono dhidi ya Southampton na hii leo watakuwa na kibarua kizito pale Villa Park yenye kocha mpya Unai Emiry.

Liverpool wapo nafasi ya 6 kwenye msimamo wa ligi wakiwa wameshinda mechi zao sita kati ya 14 walizocheza, sare nne kupoteza mara nne na pointi zao 22.
Wakati kwa upande wa Aston Vila wao wameshinda michezo mitano , sare tatu na wamepoteza michezo saba, pointi 18. Mechi ya mwisho kukutana Villa walipoteza mchezo leo hii nani kuondoka mbabe?

