Mgunda: "Tunahitaji Pointi 3"

Kuelekea mchezo wao wa Ligi kuu wa raundi ya 18, kati ya Simba dhidi ya KMC  kocha mkuu wa Simba Juma Mgunda amesema kuwa anahitaji pointi 3 katika mchezo huo utakaopigwa majira ya saa 10:00 jioni CCM Kirumba.

 

Mgunda: "Tunahitaji Pointi 3"

Mgunda ametoka kuchukua tuzo ya kocha bora wa mwezi uliopita na leo hii anatajiwa kuwaongoza Msimbazi kuchukua alama tatu kwa vijana wa Thierry Hitimana KMC, ambao wametoka kushinda michezo yao miwili mfululizo.

Simba ya Juma Mgunda wamechwa pointi 9 na mtani wake Yanga ambaye yupo nafasi ya kwanza baada ya kujikusanyia alama 47 na ushindi wa jana dhidi ya matajiri wa Chamazi Azam zimemfanya azidi kuwa kileleni.

Mgunda: "Tunahitaji Pointi 3"

KMC yupo nafasi ya 9 baada ya kujipatia alama 22 kwenye michezo 17 aliyocheza huku mechi ya kwanza akimlazimisha mnyama sare ya mabao 2-2 katika uwanja wa Benjamin Mkapa.

Kocha wa Simba anataka pointi tatu ili apunguze gepu lililopo kati yao na mabingwa na mabingwa watetezi kabla ya kujua kama nafasi ya kutetea taji hilo ipo laa.

 

 

 

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.