Yanga Yailambisha Azam Dozi 3

Ligi kuu ya NBC jana imepigwa michezo mitatu na wa mwisho ni ulie uliowakutanisha kati ya Yanga dhidi ya Azam katika uwanja wa Benjamin Mkapa majira ya saa 2:15 usiku yakishuhudiwa mabao 5.

 

Yanga Yailambisha Azam Dozi 3

Yanga waliipatia Azam dozi ya mabao 3-2 ambapo wananchi ndio waliosawazisha bao la kwanza la Abdul Sopu kupitia kwa mfungaji wao hodari Fiston Mayele na Aziz Ki na kwenda dakika 45 za kwanza kukiwa na mabao matatu.

Baada ya wananchi kwenda maumziko wakiwa na uongozi wa mabao 2-1, waliporejea tu kipindi cha pili Sopu anaingia kamabni mara ya pili na kufanya ubao usomeke 2-2 huku kukiwa na mashambulizi ya kila pande.

Yanga Yailambisha Azam Dozi 3

Dakika ya 77 Faridi Mussa anatumia ufanisi na kosa la golikipa Ahmada na kupachika bao la kuwapa Yanga pointi 3 za kibabe katika Derby hiyo ya Mzizima na kuwafanya wanalamba lamba waambulie patupu licha ya kufanya majaribio mengi.

Hivyo kutokana na matokeo hayo vijana wa Nabi wanaendelea kukaa kileleni kwenye msimamo wa NBC wakiwa wamejikusanyia pointi zao 47, pia Mayele akifikisha bao lake la 14 baada ya kufunga jana.

Yanga Yailambisha Azam Dozi 3

Azam FC ya Kally Ongala sasa wamefikisha mechi 3 bila ya kupata pointi 3 ambapo kati ya hizo mechi wametoa sare mbili na kupoteza jana.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.