Lewandowski: Messi Yupo kwenye Nafasi Nzuri ya Kushinda Ballon Dor

Mshambuliaji wa klabu ya Fc Barcelona Roberto Lewandowski anaamini staa wa klabu ya PSG  na timu ya taifa ya Argentina Lionel Messi yupo kwenye nafasi nzuri zaidi ya kushinda tuzo ya Ballon Dor mwaka huu 2022.

Staa Lionel ambaye amekua kwenye kiwango bora sana na klabu yake ya PSG akifanikiwa kuhusika kwenye mabao mengi msimu huu, Huku ikiwa tofauti sana na msimu uliomalizika ambapo mchezaji huyo alikua na msimu mbaya ndani ya klabu hiyo.lewandowskiMshambuliaji Lewandowski anaamini Messi yupo kwenye nafasi nzuri zaidi ya kushinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia maarufu kama Ballon Dor kutokana na kiwango bora alichokionesha kwenye michuano ya kombe la dunia mwaka huu nchini Qatar.

Lionel Messi amefanikiwa kuhakikisha anaiwezesha timu yake ya taifa ya Argentina inashinda taji la kombe la dunia nchini Qatar, Huku yeye akiwa na kiwango bora sana na akifanikiwa kushinda tuzo ya mchezaji bora wa michuano hiyo mwaka huu.lewandowskiStaa Lewandowski anaamini kipimo kikubwa cha mchezaji kupewa tuzo ya mchezaji bora wa dunia itakua michuano ya kombe la dunia, Hivo anaamini kwa kiwango alichoonesha Lionel Messi kwenye michuano hiyo ni wazi kabisa yupo kwenye nafasi nzuri zaidi ya kutwaa tuzo yake ya nane ya Ballon Dor.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.