Mgunda kuwarejesha fasta nyota Simba mazoezini

Baada ya kupata sare ya bao 1-1 dhidi ya Kagera Sugar jana jumatano, Kocha Mkuu wa Simba amesema wanaenda kuyafanyia kazi mapungufu yaliyopo kwenye kikosi mara baada ya kurejea mazoezini.

Kikosi cha Simba leo kimeondoka Bukoba kuelekea mkoani Mwanza kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa ligi dhidi ya KMC ambao utapigwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Mgunda kuwarejesha fasta nyota Simba mazoezini

Akizungumzia mipango yao, Mgunda amesema “Ni kweli tumepoteza pointi mbili tukiwa ugenini tumefanya kosa moja la kutokuwa makini na wenzetu wamelitumia.

“Tuna siku kadhaa za kujiandaa na mchezo ujao dhidi ya KMC hivyo tunaenda kurekebisha yale mapungufu yaliyojitokeza kwenye mchezo wa jana.”

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.