Mabingwa wa Uefa conference league Chelsea wameonesha uhitaji wa golikipa wa Ac Milan, Mike Maignan huku kocha Enzo Maresca akionesha nia ya kuwa na golikipa namba moja ndani ya kikosi chake kuelekea msimu ujao.

Maignan anamaliza mkataba wake na Milan tarehe 30 mwezi huu na inasemekana mpaka sasa bado hajaamua kuongeza mkataba.
Inaelezwa kwamba Maigan anatamani kucheza Klabu bingwa Ulaya na kujitengenezea nafasi kwa timu ya taifa ya Ufaransa, hivyo Ac Milan wanakosa nafasi ya kuendelea nae baada ya kushinda kufuzu kwa ajili ya michuano hiyo kwani wamemaliza nafasi ya nane kwenye msimamo wa ligi.
Kiwango alichokionesha golikipa Robert Sanchez ndani ya Chelsea kimeibua mshtuko miongoni mwa maboss wa timu hiyo hali inayowafanya kuhakikisha waanapata mbadala wake mapema kuelekea michuano ya Ligi ya mabingwa watakayoshiriki msimu ujao mara baada ya kufanikiwa kumaliza ndani ya nafasi tano za msimamo wa ligi kuu nchini Uingereza.


