Christian Pulisic mwenye miaka 24, ni mmoja wa nyota ambao huenda wakaondolewa na Chelsea msimu huu wa joto huku gazeti la Daily Mail likisema anaweza kutumiwa kuvutia jina jingine kubwa Stamford Bridge.

Mshambuliaji huyo wa Marekani anaweza kutumika kama sehemu ya makubaliano ya kuishawishi Napoli kumuuza mshambuliaji wa Nigeria Victor Osimhen.
Paris Saint Germain wako tayari kuwasilisha ombi la kutaka kumnunua winga wa Crystal Palace Michael Olise, 21. Gazeti la Daily Mail linaripoti kwamba miamba hao wa Ligue 1 watafanya uhamisho wa kumnunua mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa chini ya umri wa miaka 21 msimu wa joto.
Kiungo wa kati wa Arsenal Granit Xhaka, 30, analengwa na Bayer Leverkusen, kulingana na Daily Mirror. Klabu hiyo ya Ujerumani ilijaribu kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Uswizi msimu uliopita wa joto na gazeti la The Sun linaripoti kuwa The Gunners wana hamu ya kumpata winga wa Leverkusen Moussa Diaby mwenye miaka 23.

Mchezaji nyota wa Blackburn Adam Wharton anavutia Newcastle, linaripoti Daily Mail. Maafisa wakuu kutoka katika klabu hiyo ya Ligi ya Premia wamekuwa wakimtazama kiungo huyo mwenye umri wa miaka 18.
Moussa Dembele pia anasakwa na Aston Villa, Leeds na West Ham wamehusishwa na kutaka kumnunua fowadi huyo wa Ufaransa, 26, kutoka Lyon.

Matteo Guendouzi ambaye ni kiungo wa kati wa zamani wa Marseille wa Arsenal mwenye miaka 24, ameibuka kama mbadala wa Declan Rice huko West Ham.

