Bruno Fernandes amemwagia sifa kemkem mchezaji mwenzake wa Manchester United David De Gea, akidai kuwa kipa huyo alistahili kuagwa kitofauti.

De Gea alifichua Jumamosi kwamba ataondoka katika klabu hiyo baada ya mkataba wake kukamilika mwishoni mwa Juni.
Na Fernandes anadai kuwa kuaga mbele ya mashabiki wa Old Trafford kungekuwa sahihi zaidi kwa mchezaji huyo aliyecheza nafasi ya tatu katika Ligi Kuu ya Uingereza.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno aliandika kwenye Instagram: “Unajua ninachofikiria kuhusu wewe na ni kiasi gani nitakukosa kaka. Ulistahili kuagwa kwenye uwanja na mashabiki wote wakishangilia kwa kumbukumbu zote nzuri.”

“Uliweka historia kwenye klabu na jina lako halitasahaulika. Kila la kheri kwa kile kitakachokuja kwako na familia yako.”
De Gea anaondoka klabuni hapo kwa kasi, baada ya kushinda Golden Glove ya Ligi Kuu msimu uliopita.
United wanadaiwa kutaka kumbadilisha na kumchukua mlinda mlango wa Inter Milan Andre Onana.

