Bruno Fernandes Anamvutia Ten Hag

Kiungo wa klabu ya Manchester United Bruno Fernandes anamkosha kocha wa klabu hiyo Erik Ten Hag kutokana na kucheza kwa hisia anapokua uwanjani japo anaona anatakiwa kuweka usawa.

Kiungo Bruno Fernandes amekua kwenye kiwango kikubwa ndani ya klabu ya Manchester United japo amekua akikosolewa mara kwa mara kwasasa na mashabiki wa klabu hiyo, Ikiwa wanadai kiwango cha kiungo kimeshuka lakini kocha wa klabu hiyo anavutiwa na kiungo huyo.Bruno fernandesKiungo huyo amekua akicheza mara nyingi akionekana mwenye hisia lakini kocha Ten Hag amekua akifurahishwa na namna anavyotumia hisia zake katika kuhakikisha anacheza vizuri kiwanjani, Lakini vilevile kocha huyo anaona kuna haja ya kiungo huyo kupunguza hisia au kuweka usawa katika hilo.

Kiungo Bruno Fernandes amekua akikosolewa baada ya mchezo dhidi ya Liverpool na mashabiki wa klabu hiyo wakieleza kua mchezaji huyo hafai kua kiongozi wa klabu hiyo, Lakini kocha Ten Hag vilevile alimtetea mchezaji wake na kusema ataendelea kua nahodha msaidizi ndani ya kikosi hicho.Bruno fernandesBruno Fernandes amekua akionesha uwezo mkubwa tangu ajiunge na klabu ya Manchester United mwaka 2020 mwezi Januari, Jambo ambalo limekua likimhukumu kwa kiasi kikubwa pale ambapo anakua anaonesha kiwango cha kiwango cha chini lakini kwa kiwango kikubwa amekua akionesha ubora mkubwa.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.