Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amesema alishangazwa na kitendo cha mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil Roberto Firmino kuamua kuondoka ndani ya klabu hiyo baada ya kukaa klabun hapo kwa muda mrefu.

Mshambuliaji Firmino aliiambia klabu yake ya Liverpool mwishoni mwa wiki iliyomalizika kua anataka kuondoka ndani ya klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu ambapo mkataba wake utakua unamalizika na kuamua kuondoka klabuni hapo kitu ambacho kilimshtua kocha wake Jurgen Klopp.kloppMshambuliaji Roberto Firmino ambaye amekua ndani ya klabu ya Liverpool kwa miaka saba sasa na kua moja ya kipenzi cha mashabiki wa Liverpool kwa kipindi ameitumikia klabu hiyo, Lakini maamuzi yake yamekuja ghafla sana kwani ilielezwa klabu yake ilikua kwenye mpango wa kumuongezea mkataba mpya.

Kocha Klopp wakati anafanya mazungumzo na wanahabari alipoulizwa kuhusu kushustushwa na taarifa ya Firmino kuondoka kocha huyo alikiri kushtushwa lakini ameweka wazi anaheshimu maamuzi ya mshambuliaji, Huku akisema ni kawaida kutokea kwa mchezaji kufanya maamuzi kama hayo.kloppRoberto Firmino amekua kwenye kiwango bora ndani ya Liverpool alifanikiwa na klabu hiyo kiwango kikubwa huku akitengeneza moja ya safu hatari ya ushambuliaji kwenye historia ya ligi kuu ya Uingereza akishirikiana na Sadio Mane, pamoja na Mohamed Salah, Vilevile akiingia kwenye orodha ya wafungaji bora wa muda wote wa klabu hiyo kwenye ligi kuu ya Uingereza.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa