Kiungo wa klabu ya Manchester United raia wa kimataifa wa Ureno Bruno Fernandes amesema anatarajia ushindani mkubwa katika mchezo wa fainali wa kombe la Carabao hapo kesho kutoka kwa klabu ya Newcastle.
Bruno Fernandes anaamini kiwango cha klabu ya Newcastle United msimu huu kimeimarika ghafla na kushangaza wengi, Huku akiiona klabu hiyo ikienda kutoa ushindani mkubwa kesho katika mchezo wa fainali utakaopigwa katika dimba la Wembley.Klabu ya Newcastle United imekua kwenye kiwango bora sana msimu huu na kufanya ambayo hayakutarajiwa na wengi kitu ambacho kinafanya kiungo huyo wa Man United kuamini kua klabu hiyo inakwenda kuwapa ushindani mkubwa katika mchezo wao.
Wakati Bruno Fernandes anaongea na waandishi wa habari alisema “Nafikiri kila mtu anajua kua Newcastle ni timu ambayo imeshangaza wengi, Sio kwasababu ya ubora wao hapana kwasababu ubora wanao kila siku, Lakini kitendo cha kupambana kubaki ligi kuu msimu uliomalizika na msimu huu wanafanya vizuri”Bruno Fernandes aliendelea kwa kusema “Nafikiri kila mtu anajua kua Newcastle ni timu ngumu msimu huu, timu iliyoruhusu mabao machache zaidi kama sio wakwanza basi watakua washika nafasi ya pili” Lakini kiungo huyo alisisitiza kua suala la msingi kwa upande wao ni kuangalia namna gani wataidhibiti Newcastle na kutwaa taji kesho.