Guardiola: "De Bruyne Hazuiliki"

Kocha mkuu wa Manchester City, Pep Guardiola amedai Kevin De Bruyne ameonyesha kuwa “hawezi kuzuilika” alipocheza hapo jana kwenye mchezo wa Kombe la Carabao na kuilaza Liverpool kwa mabao 3-2.

 

Guardiola: "De Bruyne Hazuiliki"

De Bruyne alikuwa chini ya kiwango chake bora wakati Ubelgiji ilipotolewa kwenye Kombe la Dunia katika hatua ya makundi mapema mwezi huu. Lakini mechi yake ya kwanza kurejea City ilitoa ukumbusho wa kipaji cha ajabu cha kiungo huyo.

De Bruyne alitoa pasi za mabao kwa Erling Haaland na Nathan Ake katika ushindi huo wa kusisimua, akitengeneza nafasi tano za juu katika mchezo alipokuwa akicheza jana katika uwanja wa Etihad.

Guardiola aliiambia Sky Sports: “Kevin, anapocheza anakuwa wa moto sana na anajipata kabisa akiwa wa moto…huyu ni mchezaji wa hatari sana.

Guardiola: "De Bruyne Hazuiliki"

Guardiola hakuishia hapo pia aliuliza kuwa Kevin yupo City kwa miaka mingapi? Saba, nane? anafikiri hivyo kuna mambo mengi sana kwani yeye ni gwiji kabisa. Siku zote anamsukuma kufanya vizuri zaidi zaidi, katika michezo muhimu anapokuwa na hii hawezi kuzuilika.

Pep alihifadhi sifa za ziada kwa Lewis, beki wa kulia mwenye umri wa miaka 18 ambaye ameonyesha kiwango kizuri katika mechi ambazo amecheza. Na amesema kuwa ni kwa muda mrefu sana, hakuona uchezaji kama Rico Lewis.

Guardiola: "De Bruyne Hazuiliki"

Rico ana umri wa miaka 18, anacheza dhidi ya Liverpool akiwa na nyota wakubwa mbele, na jinsi alivyocheza na mpira na bila mpira. Wana bahati, bahati nzuri kuwa na mchezaji huyu kwa muongo ujao, na wanatumai klabu inaweza kumbakisha, kwa sababu alikuwa wa kipekee. Mchezo aliocheza ulikuwa wa kipekee.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.