Mchezaji wa Manchester United Cristiano Ronaldo amekiri kuwa alikaribia kujiunga na Manchester City mnamo 2021 kabla ya kuamua kurejea katika klabu ya zamani Manchester United.
Ronaldo alikuwa akiondoka Juventus, huku klabu hiyo ya Serie A ikiripotiwa kuwa na hamu ya kupata mshahara wa mchezaji huyo wa Kimataifa wa Ureno wakati huo, na kwa kushangaza alikuwa akihusishwa na kuhamia kwa mabingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza Pep Guardiola.
Akiongea na Piers Morgan kwenye TalkTV, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 37 alielezea kwa kina mabadiliko yaliyomalizika kwa yeye kurejea Old Trafford miaka 12 baada ya kuondoka kwenda Real Madrid.
Ronaldo alisema kuwa; “Kusema kweli, ilikuwa karibu kuhamia City” na walizungumza mengi na Guardiola na kusema kuwa wiki mbili zilizopita walijaribu sana kumpata.
Lakini mchezaji huyo aliendelea kusema kuwa historia yake na Manchester United, moyo wake, na hisia zake, historia ambayo aliifanya hapo awali ilileta mabadiliko na bila shaka pia walizungumza na Sir Alex Ferguson.
Licha ya moyo wake mkubwa, Ronaldo hakuweza kuirejesha United kwenye ubora wake wa zamani, ingawa kwa kiasi fulani alikosa juhudi kwani alifunga mabao 18 kwenye ligi lakini timu hiyo ilimaliza katika nafasi ya sita ikiwa na pointi zao za chini kabisa katika historia ya Ligi Kuu.
Pia aliongea kuhusu athari alizofanya aliporejea mara ya kwanza, huku Morgan akimuuliza kuhusu jezi zake mfano wa jezi za Lionel Messi baada ya kuhamia Paris Saint-Germain.
Hakusita kusema kuwa; “Bila shaka nilifurahishwa na hilo, kama unavyojua mimi sifuati rekodi, rekodi zinanifuata.”
Wakati watu wengi wakitarajia Ronaldo kutua pale Etihad, mambo yalibadilika baada ya masaa 72 ambapo sio City pekee bali vilabu vingine pia kutokana na uhamishpo huo na pia alisema ilimshamngaza kila mtu, na hata yeye pia.