Mchezaji wa Manchester United na timu ya Taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo hatacheza mechi ya Ureno ya kujiandaa na Kombe la Dunia dhidi ya Nigeria siku ya leo kwa sababu ya ugonjwa na kocha wa Taifa hilo amethibitisha.

 

Ronaldo Kuikosa Nigeria Leo

Fernando Santos ambaye ndiye kocha mkuu wa Ureno  ametupilia mbali wasiwasi kuhusu mahojiano ya Ronaldo na Piers Morgan ambapo aliikosoa klabu yake, Manchester United akisema kuwa haimtendei haki.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Santos alisema: “Ronaldo ana ugonjwa wa gastritis na hakufanya mazoezi leo ili kupata nafuu na kupumzika, na ni hali ambayo haisaidii sana kwani inawaathiri sana wachezaji, wanaopoteza kimiminika kingi, na wanadhoofika.”

Ronaldo Kuikosa Nigeria Leo

Kocha huyo alisisitiza kuwa Ronaldo hatakuwepo kwenye mchezo wa leo wa kirafiki watakaocheza dhidi ya Nigeria huku akisema kuwa haina haja ya kuwafahamisha kuhusu mahojiano yake kwani yeye yupo huru kufanya maamuzi yake.

Santos amesema kuwa anachovutiwa nacho ni yale yanayozungumzwa katika kambi yao na sio yale yanayosemwa nje, na wanapaswa kuheshimu uamuzi wake. Pia alisisitiza kwa kusema kuwa wapaswa kuheshimu mahojiano aliyotoa na hayana uhusiano na timu ya Taifa.

Ronaldo Kuikosa Nigeria Leo

Ureno wataanza kampeni zao za Kombe la Dunia dhidi ya Ghana mnamo Novemba 24, kabla ya kumenyana na Uruguay na Korea Kusini katika Kundi H.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa