Mshambuliaji wa klabu ya Simba Mosses Phiri awamaliza Namungo baada ya kufunga bao ambalo liliipa Wekundu wa Msimbazi pointi 3 muhimu walipokuwa wakicheza mchezo wao wa raundi ya 11.

 

Phiri Awamaliza Namungo

Mchezo huo ulipigwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa majira ya saa 1:00 usiku na ndipo ndani ya dakika ya 31 Phiri anapokea krosi safi kutoka kwa mlinzi wa pembeni wa Simba Mohamed Zimbwe na kupachika kambani bao hilo.

Dakika 45 za mwanzo zilikamilika kwa Phiri kuitanguliza mbele Simba kwa bao 1-0, licha ya  Wekundu hao kukosa nafasi za wazi kadhaa ikiwemo ile aliyokosa Kibu Denis ambayo ingewafanya waongoze kwa mbao 2-0.

Waliporudi katika kumalizia dakika 45 za pili Namungo nao walifunguka japo wapate bao la kusawazisha lakini mambo yalikuwa magumu kwani eneo lao la ushambuliaji walikosa watu wafanisi na kocha akashindwa kumuingiza Lusajo mapema ambaye ndiye kinara wao wa mabao.

Phiri Awamaliza Namungo

Baada ya Blessings kutoka na kuingia Lusajo Namungo walionekana kuwa hatari zaidi lakini lakini muda ulikuwa umewatupa mkono na kuwafanya wapoteze kwa bao moja kwa bila na kushuka kutoka nafasi ya 6 hadi ya nane kwenye msimamo.

Tangu Namungo apande Ligi kuu Tanzania Bara 2019  hajawahi kuifunga Simba, mechi 07 walizokutana Namungo kapoteza 5 kapata sare mbili.

Phiri anafikisha mabao 6 kwenye Ligi akiwa sawa na Reliants Lusajo, huku akiwa nyuma ya bao moja kwa mchezaji wa Mbeya City Sixtus Sabilo mwenye mabao 07.

Phiri Awamaliza Namungo

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa