Mchezo wa simba na singida unakwenda kupigwa hapo kesho huku kiingilio cha kuwaona nyota hawa Meddie Kagere wa Singida Big Stars na Moses Phiri wa Simba kwenye mchezo wa ligi ni 5000 tu kwa siti za mzunguko.

Mchezo huo wa ligi unaokutanisha timu hizo utapigwa kwenye Uwanja wa Liti,  mkoani Singida ukiwa ni mchezo wa kwanza kwa timu hizo kukutana msimu huu ndani ya NBC Premier League

Viingilio vya mzunguko ni 5000 huku viingilio vya VIP vikiwa ni 10000 pekee katika mchezo huo.

Singida wanashuka kwenye mchezo huo wakiwa na kumbukumbu ya kuvuna pointi tatu dhidi ya Polisi Tanzania huku Simba wakizivuna dhidi ya Mtibwa Sugar.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa