Simba SC: Baada ya ushindi mkubwa kwa mara kwanza msimu huu wa mabao 5-0 dhidi ya Mtibwa Sugar ya mkoani Morogoro, sasa watarejea uwanjani kucheza na timu yenye Wabrazil wengi, Singida Big Star.

Mchezo huo unatarajiwa kupigwa kwenye uwanja wa Liti, mkoani Singida ambao ni uwanja wa nyumbani wa timu hiyo inayofanya vizuri kwa sasa ikiwa kwenye nafasi ya 7, na alama 14, nyuma ya Mtibwa, Namungo, Mbeya City, Azam, Simba na Yanga anayeongoza Ligi kwa sasa.
Kwa upande wa kikosi cha Simba tayari kimeanza mazoezi ya kujiandaa na mchezo huo, huku kiungo katili Sadio Kanoute akijiunga na wenzake baada ya kupona majeraha yaliyomuweka nje kuanzia mechi ya Kariakoo Derby, hivyo alizikosa mechi 3 na timu yake.

Endapo Simba akishinda mchezo huo atakuwa na alama 20, sawa na Yanga SC lakini atakuwa amemzidi mpinzani wake mchezo mmoja.

Ulishawahi kuwaza kuwa rubani wa maisha yako!! Kuwa rubani wa mchezo pendwa wa Aviator wa kasino mtandaoni. Aviator bonanza inazidi kutoa michongo ya mkwanja kwenye nyumba ya mabingwa. Unarusha ndege yako na unashinda, kuwa rubani wa kujivunia kwa kuibuka na mkwanja leo.

