Simba: Phiri Yeye na Ligi ya Mabingwa Tu

Mshambuliaji wa Simba Moses Phiri amesema kuwa  kwa sasa akili yake inawaza kusaidia Simba kuweza kufika mbali zaidi kwenye michuano ya kimataifa huku akitamanai kuwa mmoja wa wachezaji watakaoweka historia ya ufungaji bora katika michuano hiyo.

Phiri kwa sasa ndani ya Simba amefanikiwa kuifungia timu hiyo mabao 5 katika michuano ya ligi ya mabingwa Afrika ambapo aliyafunga mara matatu katika michezo miwili dhidi ya Nyassa Big Bullet na mawili dhidi ya De Agosto.

Phiri alisema kuwa anafuraha kuona kuwa Simba imeweza kufanikiwa kutinga katika hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa Afrika huku akitamba kuhitaji kuweka historia ya ufungaji bora ndani ya Simba katika michuano hiyo na kuifikisha mbali zaidi.

“Furaha yetu kubwa ni kuona tumeweza kutinga hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa Afrika msimu huu,malengo yangu kwa sasa ni kuona naisaidia Simba kufika mbali zaidi katika michuano hii mikubwa ya Afrika.

“Kwangu binafsi pia natamani kuona nakuwa mmona kati ya wachezaji watakaoweka historia ya kufunga mabao mengi zaidi kutokea Simba katika michuano hii,kuwa mfungaji bora pia ni ndoto kubwa kwangu naamini kila kitu kinawezekana,ni malengo na jitihada,” alisema mshambuliaji huyo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.