Mchezaji wa Yanga, Stephane Aziz Ki na Clatous Chama wa Simba wameipa bodi ya ligi Mil 1 baada ya kutozwa faini kwa kosa la kukwepa kusalimiana na wachezaji wa timu pinzani.

Tukio hilo lilitokea Oktoba 23 mwaka huu kwenye mchezo wa ligi kati ya Yanga na Simba uliopigwa kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar na kumalizika kwa sare ya bao 1-1.

Aziz Ki, Aziz Ki na Chama Wapigwa Faini ya Milioni 1 na Bodi ya Ligi, Meridianbet

Pia wachezaji hao wamefungiwa michezo mitatu kila mmoja kutokana na kosa hilo.

Kupitia taarifa kutoka bodi ya ligi kuu, imeeleza kuwa|: “Kamati ya uendeshaji na usimamizi wa ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania imewafungia michezo mitatu na faini ya Shilingi 500,000 wachezaji Stephane Aziz Ki wa Yanga na Clatous Chama wa Simba kwa kosa la kukwepa kusalimiana na wachezaji wa timu pinzani kabla ya mechi yao ya Oktoba 23, 2022.”

Pia klabu ya Yanga imetozwa faini ya Shilingi Milioni tano (5,000,000) kwa kosa la kutotumia mlango rasmi wakati wakiingia chumba cha kuvalia.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa