Aliyekuwa straika wa Simba, Meddie Kagere ambaye kwa sasa anakitumikia kikosi cha Singida Big Stars ameanza kufunga mabao ligi kuu.
Kagere alijiunga na Singida Big Stars kwenye dirisha kubwa la usajili la msimu huu akitokea Simba baada ya mkataba wake kuvunjwa.

Nyota huyo tangu ajiunge na kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, Hans Van De Pluijim hakuwahi kufunga bao lolote kwenye ligi.
Jana jumapili kikosi cha Singida Big Stars kilimenyana na Polisi Tanzania ambapo Meddie Kagere ndiye alifanikiwa kuifungia bao pekee la ushindi timu yake.
Mchezo huo ulipigwa kwenye Uwanja wa Black Rhino Academy uliopo Karatu, Arusha ambao ulimalizika kwa Singida kuibuka na ushindi wa bao 1-0.

