Mchezo huo wa ligi unatarajiwa kupigwa kesho jumatano kwenye Uwanja wa Liti, Singida ambapo Singida Big Stars watakuwa wenyeji wa mchezo huo.
Kikosi cha Simba kiliondoka Dar jana jumatatu kuelekea mkoani Singida kwa ajili ya mchezo huo ambapo leo kinatarajia kufanya maandalizi ya mwisho.
Mgunda alisema kuwa: “Wachezaji wote tulioondoka nao wapo fiti tayari kwa ajili ya mchezo huo wa ligi kuu dhidi ya Singida Big Stars.
“Tunajua Singida wana wachezaji wazuri na ukizingatia aina ya pia wapo kwenye Uwanja wao wa nyumbani hivyo mchezo utakuwa mgumu sana.
“Sisi tunaingia kwenye mchezo huo kwa tahadhari kubwa kwa ajili ya kuhakikisha tunapata ushindi kwenye mchezo huo kulingana na aina ya kikosi tunachoenda kukutana nacho.”