Ushindi wa Mbeya City hii leo utamfanya apande hadi nafasi ya 4 ya Ligi kuu ya Tanzania endapo ataweza kumfunga Kagera Sugar baada ya kutoka kulazimishwa sare ya kufungana mchezo uliopita.

 

Je Mbeya City Kupanda Nafasi ya 4 Leo?

Mbeya City atakuwa katika Dimba la Sokoine jiji Mbeya kumenyana na vijana wa Mecky Mexime waliotoka kupoteza pointi tatu dhidi ya mabingwa watetezi Yanga, sasa hii leo wataenda kujiuliza dhidi ya Wanakoma kumwanya.

Sixtus Sabilo na wachezaji wenzake wapo nafasi ya saba baada ya kucheza michezo 10, ushindi matra 4 sare 4, na kupoteza mara mbili huku wakijikusanyia point 16 kibindoni. Wakati Kagera wao wanashikilia nafasi ya 13 michezo 11 ushindi mara nne, sare mbili na kupoteza mara 6.

Je Mbeya City Kupanda Nafasi ya 4 Leo?

Kagera Sugar kwenye kuzitafuta pointi tatu ugenini leo, endapo watashinda watapanda hadi nafasi ya 9 huku wakijiondoa katika hatari ya kusguka daraja au kucheza “Play off” kwenye mwisho wa msimu.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa