Klabu ya soka ya Mbeya City kutoka jijini Mbeya imeshuka dimbani leo kumenyana na wagosi wa kaya klabu ya Coastal Union mchezo uliopigwa katika dimba la Sokoine jijini Mbeya huku mchezo ukimalizika bila mbabe.

Mchezo huo ambao ulikua wa piga nikupige ambapo klabu ya Mbeya City ambao leo walikua wenyeji wao walikua na kazi ya kusawazisha tu huku Coastal Union wakitangulia mara zote katika mchezo huo.mbeya cityMchezo huo umemalizika kwa sare ya mabao mawili kwa mawili huku magoli ya utangulizi ya klabu ya Coastal Union Greyson Gwalala na Hamad Majimengi huku magoli ya wenyeji yakifungwa na Sixtus Sabilo aleefunga magoli yote mawili ya kusawazisha.

Klabu ya Mbeya City wao wanakua wamefikisha alama 16 kwenye ligi kuu ya NBC huku Coastal wao wakifikisha alama 12 vaada ya sare ya mchezo wa leo katika dimba la Sokoine.

Mshambuliaji wa Mbeya City Sixtus Sabilo yeye ameendelea kua na msimu mzuri baada ya kufunga magoli mawili leo na kufikisha jumla ya mabao saba na kuongoza kwenye mbio za kiatu cha dhahabu msimu huu.

aviator

Ulishawahi kuwaza kuwa rubani wa maisha yako!! Kuwa rubani wa mchezo pendwa wa Aviator wa kasino mtandaoni. Aviator bonanza inazidi kutoa michongo ya mkwanja kwenye nyumba ya mabingwa. Unarusha ndege yako na unashinda, kuwa rubani wa kujivunia kwa kuibuka na mkwanja leo.

BONYEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa