Mtendaji Mkuu wa Borrusia Dortmund Hans-Joachim Watzke ameweka wazi kuwa, baada ya kumalizika kwa michuano ya kombe la dunia nchini Qatar mwaka 2022, watakaa mezani kuzungumzia suala la Mshambuliaji wa timu hiyo Jude Bellingham.

 

CEO Dortmund Avunja Ukimya Kuhusu Bellingham

Dortmund imekuwa ikizongwa na vilabu vingi barani Ulaya kuhusu mchezaji huyo Raia wa Uingereza ambaye ameitwa na Kocha wa Timu ya Taifa hilo Gareth Southgate, kuongeza nguvu kwenye safu yake ya Ushambuliaji ambayo taifa hilo linakabiliwa na mechi ya kwanza Novemba 21 Dhidi ya Iran.


Mtendaji Mkuu wa Dortmund Watzke alisema kwamba wataongea na Jude kuhusu Mustakabali wake klabuni hapo.

 

CEO Dortmund Avunja Ukimya Kuhusu Bellingham

“Baada ya Kombe la Dunia Qatar, tutajadili kuhusu Jude matakwa yake, anapaswa kutuambia kama atahitaji kusalia nasi au kuondoka. Kama kweli vilabu vikubwa vinahusika, pia tunaweza kushindana navyo kiuchumi” Alisema Watzke.

Jude Bellingham amekuwa na msimu mzuri sana kwenye timu hiyo inayocheza Ligi kuu ya Ujerumani Bundasliga.


Ulishawahi kuwaza kuwa rubani wa maisha yako!! Kuwa rubani wa mchezo pendwa wa Aviator wa kasino mtandaoni. Aviator bonanza inazidi kutoa michongo ya mkwanja kwenye nyumba ya mabingwa. Unarusha ndege yako na unashinda, kuwa rubani wa kujivunia kwa kuibuka na mkwanja leo.

BONYEZA HAPA

aviator


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa