Beki wa klabu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Ujerumani Antonio Rudiger amefunguka kua hakuwahi kuiweka klabu ya Barcelona kwenye mipango yake wakati anafikiria kuondoka klabu ya Chelsea majira ya joto.

Beki huyo mtata amezungumzo hay akifanyiwa mahojiano katika kituo kimoja nchini Hispania pal alipoulizwa kuhusiana na kuhitajika na klabu ya Barcelona pale ambapo mkataba wake ulikua ukielekea ukingoni, Na mchezaji huyo kuweka wazi kua ni kweli miamba hiyo ya Catalans ilihitaji huduma yake lakini akaeleza hakuiona nafasi yeyote ya yeye kujiunga na Barca.RudigerAntonio Rudiger ameeleza alikua ni mwenye furaha na maisha ndani ya Chelsea lakini pale klabu ya Real Madrid ilipomuhitaji alifurahia kwani kwenye akili yake ilikua ni klabu ya Chelsea au mabingwa hao watetezi wa ulaya, Hivo haikua kazi ngumu kwa yeye kujiunga na klabu ya Real Madrid.

Beki huyo raia wa Ujerumani aliondoka kwenye klabu ya Chelsea kutokana na mkataba wake kumalizika na mabosi wa klabu hiyo kushindwa kumuongezea kutokana na kushindwana katika malipo hivo beki huyo akaamua kutimkia ndani ya Real Madrid.rudigerRudiger amefanikiwa kuitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Ujerumani kitakachoshiriki michuano ya kombe la dunia nchini Qatar inayotarajiwa kuanza mwezi huu tarehe 20, Na beki huyo pia amekua miongoni mwa wachezaji wanaopendwa na mashabiki wa klabu ya Real Madrid.

aviator

Ulishawahi kuwaza kuwa rubani wa maisha yako!! Kuwa rubani wa mchezo pendwa wa Aviator wa kasino mtandaoni. Aviator bonanza inazidi kutoa michongo ya mkwanja kwenye nyumba ya mabingwa. Unarusha ndege yako na unashinda, kuwa rubani wa kujivunia kwa kuibuka na mkwanja leo.

BONYEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa