Klabu ya Inter Milan imefanikiwa kupata alama tatu muhimu ikiwa ugenini katika dimba la Gewiss dhidi ya Atalanta baada ya kuifunga klabu hiyo kwa jumla ya mabao matatu kwa mawili jioni ya leo.

Klabu ya hiyo baada ya kushinda mabao sita katikati ya wiki dhidi ya Bologna leo tena wameendeleza wimbi la ushindi baada ya kuifunga Atalanta na kukwea hadi nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi kuu nchini Italia.inter milanMagoli mawili ya Eden Dzeko na bao moja la kujifunga la Luis Palomino yaliiwezesha klabu hiyo kuweza kuondoka na alama tatu muhimu kabisa katika dimba la Gewiss na kuwaacha vijana wa Gian Gasperinni mdomo wazi.

Ikumbukwe klabu ya Inter Milan ilianza msimu wake vibaya na kupelekea hadi mashabiki wa klabu hiyo kutaka kocha wa klabu hiyo Simeone Inzaghi kufukuzwa lakini klabu hiyo imefanikiwa kurudi kwenye mfululizo wa kupata matokeo mazuri kama ilivyokua misimu kadhaa iliyopita.inter milanKlabu hiyo ilianza kurejesha makali yake pale ambapo walifanikiwa kupata alama tatu dhidi ya klabu ya Fc Barcelona kwenye ligi ya mabingwa barani ulaya, Ambapo walihitajika washinde mchezo huo ili waweze kufuzu hatua inayofuata.

Unaweza kusema Barcelona ndio waliwaamsha klabu ya Inter Milan kwani kuanzia mchezo ule vijana wa Simeone Inzaghi wamekua wakipata matokeo mazuri kwenye michezo yao ya ligi kuu nchini Italia Serie A.


aviator

Ulishawahi kuwaza kuwa rubani wa maisha yako!! Kuwa rubani wa mchezo pendwa wa Aviator wa kasino mtandaoni. Aviator bonanza inazidi kutoa michongo ya mkwanja kwenye nyumba ya mabingwa. Unarusha ndege yako na unashinda, kuwa rubani wa kujivunia kwa kuibuka na mkwanja leo.

BONYEZA HAPA


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa