Kocha wa Manchester United Erik ten Hag amekiri kuwa mchezaji wake Donny van de Beek lazima ajiimarishe  ili kuwa na mafanikio katika Manchester United, lakini anakataa kumkatia tamaa kiungo huyo.

 

Ten Hag Akataa Kumkatia Tamaa Van de Beek

Akiwa ameonyesha kiwango cha juu katika timu ya Ten Hag ya Ajax, Van de Beek alihamia Old Trafford kwa ada ya awali ya pauni milioni 35 mnamo 2020, lakini tangu wakati huo amekuwa na hapati nafasi ya kucheza toka utawala wa Solskjaer.

Van de Beek alicheza mechi 27 za Ligi kuu ya Uingereza katika kampeni zake mbili za kwanza akiwa na United, na amecheza kwa dakika 19 pekee kwenye mashindano msimu huu baada ya kuvumilia kipindi kigumu cha mkopo akiwa na Everton mapema 2022.

Mapambano hayo yamemfanya Van de Beek kupoteza nafasi yake kwenye kikosi cha Uholanzi kabla ya Fainali za Kombe la Dunia nchini Qatar, lakini Ten Hag ambaye alimuanzisha kiungo huyo katika ushindi wa Alhamisi wa Ligi ya Europa dhidi ya Real Sociedad  anaamini kwamba mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 anaweza kubadilisha maisha yake hapo.

Ten Hag Akataa Kumkatia Tamaa Van de Beek

Ten Hag alipoulizwa Alhamisi kama kungekuwa na wakati ambapo United walikubali uhamisho wa Van de Beek haujafanikiwa, Ten Hag alijibu: “Ndiyo, sio sasa na ninadhani alikuwa na maandalizi mazuri ya msimu mpya.”

Van de Beek alikuwa majeruhi na sasa amerejea. Wiki iliyopita dhidi ya Sheriff kwenye Ligi ya Europa anadhani alicheza vizuri sana hivyo anachotakiwa kufanya ni kuongeza juhudi tu.

Kocha huyo aliongezea kuwa mchezaji huyo anaweza kufanya vizuri zaidi kwani anamfahamu vyema, na alitoa kile ambacho alitarajia katika suala la uwekaji nafasi, na kila kitu. Pia anaweza kuwa tishio zaidi kwenye lango la wapinzani, na huo ndio ubora wake mkubwa.

Ten Hag Akataa Kumkatia Tamaa Van de Beek

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa