Wawakilishi wa Kanda ya Cecafa kwenye Mashindano ya Ligi ya Mabingwa Simba Queens, leo watakuwa na kazi moja tu, kuhakikisha wanavuna alama tatu mbele ya Green Buffaloes ya Zambia.

Simba watacheza mechi yao ya mwisho ya kundi A kesho Jumamosi, ambayo ushindi pekee ndiyo utawapa uhakika wa kuungana na AS FAR Rabat kwenye hatua ya nusu fainali na kama watafungwa ni wazi watakuwa wamebebeshwa mabegi kilazima na kurejea nyumbani.

Simba Queens, Simba Queens, Kupigana Kiume Morocco, Meridianbet

Simba wamevuna alama tatu kwenye mechi mbili walizocheza sawa na Green Buffaloes ambao watakutana leo na kwa maana hiyo timu itakayoshinda ndiyo itavuka na kuungana na AS FAR ambao hakuna cha kuwazuia kwenda nusu fainali.

Charles Lukula Ayiekho Mbuzi kocha wa Simba Queens alipozungumzia mchezo huo alisema: “Nafikiri hakuna namna nyingine nzuri ya kuweza kuzungumza jinsi tunavyoupa kipaumbele mchezo huo. Kwa sababu ndiyo umebeba hatma yetu.

“Wachezaji wote wapo tayari na tumezungumza nao, majukumu gani wanatakiwa kufanya tumewapa, kazi itabaki kuwa kwa upande wao kutimiza hilo wakiwa uwanjani.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa