Novemba 9 mwaka huu kwenye uwanja wa Liti mkoani Singida, Simba watakuwa wageni wa Singida Big Stars kwenye mwendelezo wa ligi kuu na uongozi wa Simba umekiri kuwa mechi hiyo siyo ya kitoto.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba Ahmed Ally alisema kuwa mchezo huo utakuwa mgumu sana kwa sababu licha ya ugeni na udogo wa Singida kwenye ligi, imesheheni wachezaji wengi bora na wenye uzoefu na mechi kubwa.

simba, Big Stars vs Simba ni Mchezo Dume, Meridianbet

Ahmed alisema, hakuna kiongozi, wachezaji au benchi la ufundi ambao wanaubeza mchezo huo, kwani moja ya timu ambazo zimeanza vema ligi na Singida ipo, hivyo haitakuwa rahisi kwao kupata ushindi ingawa wana Imani wa kuondoka kifua mbele.

“Mchezo huu siyo rahisi hata kidogo na hakuna mtu mmoja kati ya wanasimba ambaye anatakiwa kuwabeza Singida. Kweli ni wadogo na wageni kwenye ligi ya msimu huu.

“Lakini ni timu ambayo kusema ukweli imesheheni wachezaji wazuri na wenye experience kubwa. Tunakwenda kupambana nao na kwa uwezo wa Mungu na ubora wa kikosi chetu tunakwenda kuchukua alama tatu palepale kwao,” alisema Ahmed.

Tofauti ya Singida na Simba ni pointi tatu tu, Simba wana alama 17 na Big Stars wana pointi 14, wakiwa nafasi ya sit ana Simba kwenye nafasi ya pili.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa