Baada ya kutokuonekana kwa muda mrefu kutokana na kusumbuliwa na majeraha, hatimae Kiungo wa Simba, Sadio Kanoute amerejea kikosini.
Miongoni mwa michezo aliyokosa Kanoute ni mchezo wa watani kati ya Yanga na Simba baada ya kuugua ghafla siku moja kabla ya mchezo huo.
Akizungumzia maandalizi yao, Ofisa Habari wa Simba, Ahmed Ally alisema “Kikosi chetu tayari kimeanza mazoezi jumatano kwa ajili ya mchezo wa ligi dhidi ya Singida Big Stars.
“Majeruhi tuliokuwa nao ni Jimmyson Mwanuke na Israel Mwenda lakini wengine wote waliobakia wapo vizuri.
“Kwenye mchezo wetu uliopita tuliwakosa Augustine Okrah pamoja na Sadio Kanoute lakini wote wamepona na tayari wameanza mazoezi na wenzao.
“Singida ni timu nzuri ukiangalia aina ya wachezaji walionao ni wazuri wana uzoefu wa kutosha hivyo tunatarajia mchezo utakuwa mgumu lakini tunaenda kupambana.”