Hassan Dilunga Afunguka Mustakabali Wake Simba

Kiungo wa klabu ya Simba Hassan Dilunga ambaye kwa sasa anajiuguza majeraha yake, amesema kuwa amekuwa akiwaambia wachezaji wa timu hiyo kupambana kuwapa furaha mashabiki.

Nyota huyo ambaye alijiunga na Simba akitokea Mtibwa Sugar kwa sasa kandarasi yake imemeguka na hajaongezewa mkataba mwingine akiwa ni huru na hakutambulishwa siku ya Simba Day.

Dilunga amebainisha kuwa amekuwa akizungumza na wachezaji wa Simba muda mwingi kila wakati kwa kuwa ni familia yake ambayo anaikumbuka.

Ninaikumbuka familia yangu ya Simba, ninawapenda wachezaji wenzangu na huwa ninawasiliana nao kwa kuwaambia kwamba lazima wapambane kuwapa furaha mashabiki wa Simba na kutimiza majukumu yao.

“Wakati naumia mkataba wangu ulikuwa umesalia miezi miwili na sasa sijasaini dili jingine ila kuna jambo litatokea kwani mawasiliano bado yapo na Simba wamekuwa wakihusika kwenye matibabu yangu pamoja na watu wengine ambao wakiona hii watajua kwamba wanahusika,”

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.